TANZANIA NA ULAYA WAKUBALIANA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA.


Serikali ya Tanzania na Ujumbe wa Mabalozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.

Akiongea baada ya kikao hicho, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Kitila Mkumbo, amesema pande zote mbili zimejadili hatua zilizofikiwa katika kuboresha masuala ya sheria, kodi, utaratibu na urasimu unaowakabili wawekezaji.


"Kumetokea maendeleo katika kuboresha mazingira ya uwekezaji. Tumejadili pia hatua zaidi za kuchukua ili kuwavutia wawekezaji zaidi kutoka Umoja wa Ulaya kuja kuwekeza hapa Tanzania," amesema Waziri Mkumbo.

Ameongeza kuwa Serikali inatekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kutoa kipaumbele kwa sekta ya kilimo ili kuongeza thamani ya mazao na kuvutia uwekezaji zaidi katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa Waziri Mkumbo, mazungumzo kama haya yamekubaliwa kufanyika kila baada ya miezi sita. Kikao kinachofuata kimepangwa kufanyika tarehe 20 Februari 2027



Post a Comment