Jumla ya miradi 42 katika mkoa wa Geita, itakaguliwa, kuzinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi na mwenge wa uhuru ambao umepokelewa Leo mkoani Geita.
MKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela, Agosti 24, 2026 amepokea rasmi Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Shinyanga.
Hafla ya mapokezi imefanyika katika Kijiji cha Nyang'holongo, Kata ya Nundu, Wilaya ya Nyang'hwale.
Akizungumza baada ya kupokea mwenge huo, Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa wa Geita kwa mwaka 2026 utakimbizwa katika Halmashauri 6.
Atanzia na Halmashauri ya Nyang'hwale hadi kumalizia katika Halmashauri ya Chato, kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa.
Ameeleza kuwa wakati wa ukimbizaji wa Mwenge Mkoani Geita, utakimbizwa kwa umbali wa Kilometa 698.2.
Katika kipindi hicho jumla ya miradi 42 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 168.74 itapitiwa. Miradi hiyo itazinduliwa, kuekwa mawe ya msingi, kukaguliwa na kutembelewa.
Notification texts go here... Link
Reach out!





