Na Miza Kona, Maelezo Zanzibar
Waziri Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Masoud Ali Mohamed amesema waasisi wa Mapinduzi wamepigania na kuikomboa nchi ili kujenga misingi ya haki na kuietea maendeleo wazanzibari waweze kujitawala.
Ameyasema hayo Migombani wakati alipotembelea kaburi na kumwombea dua Marehemu Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi aliyekuwa Rais wa awamu ya Pili wa Zanzibar, amesema viongozi hao wamefanya juhudi kubwa ya kupambana na kuikomboa nchi na kuleta mafanukio na kuwa sadaka kwa kizazi cha sasa na baadae.
Amesema wazanzibari wameondokana na unyanyasaji kutokana na mchango wa waasisi hao kuamua kupigana kwa hali na mali kuikomboa nchi ili wananchi wa Zanzibar kupata haki zao ambazo walinyang’anywa na wakoloni na kukosa kuzitumia.
“Viongozi wetu hawa walipambana kuigombania nchi katika kujenga misingi ya haki na kujenga nchi yao kwa nguvu zao zote ili kihakilisha kuwa wazanzibari wanapata haki zao na kuweza kujitawala wenyewe” amefahamisha Waziri Masoud.
Aidha amefahamisha kuwa Serikali inathamini mchango wao walioutoa na wananchi wanapaswa kukumbuka juhudi zao waliozozifanya katika kuikomboa nchi na kuleta aaendeleo nchini na kusisitiza jamii kumuenzi na kuyatunza kutokana na mafanikio yaliyopatikana ili iwe urithi mzuri wa kizazi cha baadae.
“Nawaomba wanajamii wenye dhamana na wasiokuwa na dhamana waishi maisha ya mzee wetu huyu wapo waliomfamu katika maisha yake na wapo waliomfahamu kwa historia yake kutokana na maono yake na uongozi wake kiongozi wetu alipenda amani na mashirikiano na sisi tuishi kwa amani kupenda kwa nashirikiano pamoja na kuheshimu utu wa mtu”, ameeleza Waziri Masoud.
Waziri Masoud ameishuru Serikali kwa kuweka utaratibu wa kuwakumbuka na kuwaombea dua Viongozi na Waasisi wa Mapinduzi waliotangulia mbele ya haki kwani hiyo ndiyo sadaka yako itakayowasaidia kutokana na mazuri waliyoyafanya katika kuikomboa nchi.
Akitoa neno la shukurani mtoto wa Marehemu Mustafa Aboud Jumbe ameishukuru Serikali kuungana pamoja kwa ajili ya kumwombea dua Mzee wao na kumtakia msamaha na rehema kwa Allah kwa kutamini machango wake katika serikali na kusisitiza kuendelea na utararibu huo ili kurithisha vizazi vijavyo ili kukumbuka wazee waliotangulia.
Maadhimisho ya wiki ya kuwaenzi viongozi wa Kitaifa, Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa kwanza wa Chama cha Afro Shirazi ambapo kilele kitafanyika Aprili 7, 2026 Kisiwandui Wilaya ya Mjini, Unguja.
