HADI JANA WATOTO 1,309,452 WALIKUWA WAMESHAPATA CHANJO YA POLIO MWANZA

………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Zoezi la utoaji wa chanjo ya Polio katika Mkoa wa Mwanza limefanikiwa kwa kiwango kikubwa ambapo hadi jana watoto 1,309,452 walikuwa wameshapatiwa chanjo hiyo.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mratibu wa chanjo Mkoa wa Mwanza, Sia Godfrey alipokuwa akizingumza na Fullshangwe Blog kuhusiana na mwenendo wa utoaji wa huduma hiyo mkoani humo.
Amesema walitarajia kuchanja watoto 1,241,809 lakini hadi jana Machi 26, 2025 walikuwa wameshachanja watoto 1,309,452 ambapo ameeleza kuwa wamevuka lengo la wizara.
“Zoezi hili kwa mkoa wa Mwanza limekuwa na mwitikio mkubwa sana kwani wazazi wametoa ushirikiano wa kutosha”, Amesema Godfrey
Aidha, ametoa wito kwa jamii kuwa na utaratibu wa kufuatilia ratiba za chanjo za kila siku ambazo ni zakawaida ili waweze kuzipata kikamilifu.
Amesema kwa watoto ambao hawajapata chanjo wazazi wawapeleke katika vituo vya afya vilivyopo karibu ili waweze kupata huduma hiyo muhimu itakayowakinga na ugonjwa wa Polio.

Post a Comment