TANZANIA SI KISIWA, TAKWIMU ZA MAFUTA GHAFI DUNIANI ZINAJIELEZA!

Tanzania si kisiwa. Takwimu za S&P Global Platts (Aprili 2026) zinaonyesha Bei ya Mafuta Ghafi Duniani imepanda kwa 88% ndani ya Mwezi Mmoja kutokana na Mzozo wa Mashariki ya Kati. Wakati Soko la Dunia likipanda Kwa Kiwango hicho, Bei ya ndani ya Tanzania imepanda kwa 33% tu. Hii inamaanisha Serikali imevunja Makali ya Bei kwa “kubeba” (Absorb) zaidi ya Nusu ya Pigo la Dunia ili Kumlinda Mwananchi. Hatulaumu Mawimbi, tunampongeza Nahodha kwa kuimudu Meli!

Ukitaka kujua ufanisi wa Serikali, tazama Majirani. Mfumo wetu wa Uagizaji wa Pamoja (Bulk Procurement) umetuepusha na Madalali ambao wangeongeza zaidi ya Sh 500 kwa kila lita.

Ulinganifu wa Bei (Makadirio ya Aprili 2026 kwa Lita/Tsh):

✓Malawi: Sh 4,500+

✓Kenya: Sh 4,150+

✓Uganda: Sh 4,200+

✓Tanzania: Sh 3,800

Tanzania bado ina Bei tulivu na ya Ushindani zaidi Ukanda huu. Huu ndio Upendo wa Serikali kwa vitendo, si kwa Maneno!

Ni rahisi kusema “Futa kodi Zote,” lakini takwimu hazidanganyi. Ndani ya kila lita ya Mafuta, kuna Fedha inayokwenda TARURA kujenga Barabara za Vijijini na REA kupeleka Umeme kwa Wananchi. Ukifuta kodi hiyo leo, unaua Miradi ya Maendeleo nchi nzima. Serikali ya kishujaa haichagui sifa za muda mfupi (Populism); tunatibu homa ya leo huku tukijenga mwili wa kesho kupitia SGR na Bwawa la Nyerere.

Jambo la hatari zaidi Kiuchumi siyo bei, bali ni UHABA. Wakati Mataifa Jirani Vituo Vyao vimefungwa kwa kukosa Bidhaa, Tanzania mafuta yanapatikana saa 24 kila kona. Aidha, juhudi za Benki Kuu (BoT) zimeimarisha Shilingi dhidi ya Dola (ongezeko la 0.45% tu mwezi huu), kuzuia bei isifike Sh 5,000. Tunapita kwenye dhoruba tukiwa ndani ya meli imara. Gurudumu la uchumi halitasimama!

“Tanzania inapita kwenye dhoruba ya dunia tukiwa ndani ya meli imara. Huwezi kuilaumu nahodha kwa sababu kuna mawimbi baharini; unapaswa kumpongeza kwa sababu meli haijazama na inaendelea kuelekea bandari ya maendeleo. Serikali inafanya maamuzi magumu leo ili tusiwe na Taifa tegemezi kesho. Huu ndio uongozi wa kishujaa.”

 *KATIBU KIJANA* 

Post a Comment