MADAKTARI BINGWA KUPIGA KAMBI HOSPITALI YA GAKALA
Na George Maziku, Geita HOSPITALI ya Gakala iliyopo kijiji cha Masumbwe, kata ya Bukandwe, wilaya ya Mbogwe inategemea kupokea jopo la madaktari bingwa watakaotoa huduma mbalimbali kuanzia tarehe 17 Agosti, mwaka huu mpaka tarehe 21. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo Bunga Dadu Gakala wakati alipozungumza na jopo la waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake. Alisema kuwa lengo la kuendesha kambi hiyo ni kuwapunguzia wananchi wa wilaya ya Mbogwe na wilaya zingine jirani, gharama za kufuata huduma za matibabu zinazotolewa na madaktari bingwa. “Hospitali ya Gakala inawatangazia wakazi wa Masumbwe kuwa kutakuwa na madaktari bingwa kuanzia Jumatatu tarehe 17 mpaka 21, mwezi huu. Tutapokea madaktari bingwa 5 wa magonjwa ya kina mama, daktari bingwa wa watoto, daktari bingwa wa upasuaji, daktarin bingwa wa mifupa na daktari bingwa wa magonjwa ya ndani kama vile sukari, presha na magonjwa mengine yote ya ndani. “Kwahiyo tunawakaribisha sana wananchi wote wa Ma…