Wizara ya Afya itaendelea kushirikina na wadau mbali mbali wakiwemo MSI Tanzania ili kuhakikisha jamii inaelimika
Na. Mwandishi wa Wizara ya Afya Zanzibar. NAIBU Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Fatma
Kabole amesema Wizara ya Afya itaendelea kushirikina na wadau mbali mbali
wakiwemo MSI Tanzania ili kuhakikisha jamii inaelimika kwa usahihi na kuweza
kupata huduma za Afya ya uzazi bila vikwazo. Dkt Kabole ameyaeleza hayo huko Golden Tulip Malindi katika
kikao cha tathmini na muendelezo wa mradi wa Start Small ambapo alisema bado
kunachangamoto zinazoathiri upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi hasa kwa
vijana ikiwemo upotoshaji, dhana potofu kuhusiana na masuala ya uzazi wa
mpangilio. Amefahamisha kuwa mradi wa Start Small umechangia kuleta
matokeo Chanya ikiwa na pamoja na mafanikio makubwa ya kupunguza vifo
vitokanavyo na uzazi kutoka 83 mwaka 2023 hadi vifo 59 Novemba 2025. Aidha amesema katika suala la njia za uzazi wa mpango imefikia
asilimia 17.5 kwa mwaka 2024 ambapo
mwaka 2023 ilikuwa asilimia 15 huku idadi ya watumiaji wan jia za uzazi wa
mpango imeongezeka kutoka asilimia 6,9 …