OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI YA NETIBOLI YA MUUNGANO


Kocha wa Timu ya Mpira ya Pete ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) akizungumza na wachezaji wa timu wakati wa kipindi cha mapumziko katika mchezo baina yao na Timu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) uliofanyika katika Uwanja wa Amani Complezx, Zanzibar. Mchezo huo ulimalizika kwa Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuibuka na Ushindi wa Magoli 45 kwa 34.

MKurugenzi Msaidizi Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Bi. Hanifa Selengu akizungumza jambo na wachezaji wa Timu wakati wa mchezo baina ya timu hiyo na Timu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) uliofanyika katika Uwanja wa Amani Complezx, Zanzibar. Mchezo huo ulimalizika kwa Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuibuka na Ushindi wa Magoli 45 kwa 34.
Sehemu ya wachezaji wa akiba na benchi la ufundi la Timu ya Mpira wa Pete (Netiboli) ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) wakifuatilia maelekezo ya kocha wa timu hiyo Bw. Mafuru Buriro wakati wa mchezo baina ya timu hiyo na Timu ya Jeshi Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) uliofanyika katika Uwanja wa Amani Complezx, Zanzibar. Mchezo huo ulimalizika kwa Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuibuka na Ushindi wa Magoli 45 kwa 34.
(NA MPIGAPICHA WETU)

TIMU ya Mpira wa Pete (Netiboli) ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) imeendeleza wimbi la ushindi katika mashindano ya Ligi ya Muungano ya mchezo huo yanayoendelea katika Uwanja wa Amani Complex, Zanzibar.

Katika matokeo ya mechi ya leo Jumatano Januari 21, 2026, Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais imeiadhibu vikali Timu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jumla ya magoli 45 dhidi ya 34 katika mchezo ambao Ofisi hiyo ilitawalawa maeneo yote ya mchezo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo, Mchezaji wa Timu hiyo, Bi. Anna Akwilini amesema nidhamu, ushirikiano na kujitumu kwa wachezaji ndio siri kubwa ya mafanikio ya timu hiyo katika mashindano hayo.

“Benchi la ufundi kupitia Kocha amekuwa akiturekebisha kwa makosa madogo madogo na pia hamasa ya mashabiki katika majukwaa imekuwa ikitujengea hali ya kujiamini na kupata hamasa kubwa katika kila mchezo tunaocheza” amesema Akwilini.

Amesema wachezaji wa timu hiyo wamekusudia kuendelea kufanya vizuri zaidi katika michezo yote iliyosalia ili iweze kuibua na ushindi na hatimaye kunyakua ubingwa wa Ligi hiyo ambayo imekuwa na ushindani wa hali ya juu kutoka kwa timu zote.

“Ofisi itahakikisha itajipanga vyema zaidi kwa kufanya usajili wa wachezaji wakati wa Ligi ya mashindano ya mchezo kwa upande wa Tanzania Bara na baadaye kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya Muungano” amesema Mwasamale.

Kwa upande wake Kocha wa Timu hiyo, Bw. Mafuru Buriro amesema mechi hiyo ilikuwa ngumu lakini kutokana uimara wa kikosi chake kimeweza kufanya vizuri na kuwa na imejipanga inapata matokeo mazuri katika michezo iliyosalia.

“JKT ni timu iliyokaa pamoja kwa muda mrefu wamezoeana na kupata muda mwingi wa kufanya mazoezi ya pamoja lakini tulitumia uzoefu na bidi ya wachezaji wetu katika kupata ushindi katika mchezo huu” amesema Buriro.

Mashindano hayo yaliyoanza tarehe 15 Januari mwaka huu yameshirikisha jumla ya Timu 11 ikiwemo Timu 06 kutoka Tanzania Bara na Timu 05 kutoka Zanzibar ambapo yanatarajia kuhitimishwa rasmi tarehe 24 Januari mwaka huu.

 Timu zinazoshiriki Ligi ya Mashindano hayo ni Ofisi ya Makamu wa Rais, JKT, JKU, Mafunzo, Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Kikosi cha Valantia Zanzibar (KVZ), Polisi Arusha, Dodoma Jiji, Zimamoto na Uhamiaji.

Post a Comment