Wizara ya Afya itaendelea kushirikina na wadau mbali mbali wakiwemo MSI Tanzania ili kuhakikisha jamii inaelimika

Na. Mwandishi wa Wizara ya Afya Zanzibar.

NAIBU Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Fatma Kabole amesema Wizara ya Afya itaendelea kushirikina na wadau mbali mbali wakiwemo MSI Tanzania ili kuhakikisha jamii inaelimika kwa usahihi na kuweza kupata huduma za Afya ya uzazi bila vikwazo.

Dkt Kabole ameyaeleza hayo huko Golden Tulip Malindi katika kikao cha tathmini na muendelezo wa mradi wa Start Small ambapo alisema bado kunachangamoto zinazoathiri upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi hasa kwa vijana ikiwemo upotoshaji, dhana potofu kuhusiana na masuala ya uzazi wa mpangilio.

Amefahamisha kuwa mradi wa Start Small umechangia kuleta matokeo Chanya ikiwa na pamoja na mafanikio makubwa ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka 83 mwaka 2023 hadi vifo 59 Novemba 2025.

Aidha amesema katika suala la njia za uzazi wa mpango imefikia asilimia 17.5 kwa  mwaka 2024 ambapo mwaka 2023 ilikuwa asilimia 15 huku idadi ya watumiaji wan jia za uzazi wa mpango imeongezeka kutoka asilimia 6,9 mwaka 2024 hadi kufikia asilimia 7.4 mwaka 2025.

Amesema kwa upande wa matumizi ya njia ya uzazi wa mpango kwa vijana yameongezeka kutoka 3581 mwaka 2024 na kufikia 5003 mwaka 2024.

Kwa upande wake Meneja Kitengo Shirikishi Afya ya uzazi na mtoto Dkt Kamilia Ali . kwa vijana na masuala mazima ya uzazi wa mpango.

Amefahamisha kuwa bado suala la uzazi wa mpango ni changamoto kwa visiwa vya Zanzibar na kwa mujibu wa WHO uzazi wa mpango ukitumika vizuri unasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 30 na kupitia mradi huo wameweza kufanya kazi kupitia huduma mkoba katika hospitali na vituo vya Afya na kufanya mafunzo kwa vitendo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Operesheni na Huduma za Afya MSI Tanzania Dkt Stephen Mutegeki amesema mradi huo umeweza kufanikisha kuwaweka vijana kwa pamoja kupitia club mbali mbali maskulini na mitaani ikiwa na lengo   kuimarisha Afya za vijana sambamba na kuepuka unyanyapaa.

Amesema wataendelea kushirkina na Zanzibar katika sekta tofauti ikiwemo afya, elimu ili kuhakikisha kuwa huduma kwa vijana zinaimarika na wanayafikia makundi yote kwa kuwapata huduma na taaluma  kuwa na taifa lenye afya.

Kwa upande wa wanufaika wa mradi huo ambao ni pamoja na ZAFAYKO, na club mbali mbali wamesema wamefanikiwa kuwafikia vijana zaidi ya elfu 50 katika kuwapatia elimu ikimo ya Afya uzazi kwa vijana, ujasiri amali.

Wamefahamisha kuwa kupitia Mradi wa MSI Tanzania umeweza kuwasaidia kujitambua, na kupata elimu juu ya Afya uzazi kwa vijana na kuwaelimisha wengine.

Mwisho

Post a Comment