Baraza la Vijana linapatiwa Jengo lenye hadhi Bora ili kutekeleza majukumu yao

Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Mhe. Shaaban Ali Othman amesema atahakikisha Baraza la Vijana linapatiwa Jengo lenye hadhi Bora  ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.

Ameyasema hayo wakati  Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Uwezeshaji walipotembelea Baraza la Vijana Mwanakwerekwe mara baada ya kikao cha kujadili  mafanikio na changamoto za Wizara hiyo klichafanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi , Chukwani.

Amesema lengo la kuanzisha Wizara ya Vijana ni kuhakikisha Ustawi bora wa Maendeleo ya Vijana unaimarika kwa kuwaletea mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kuwaodoshea changamoto za awali ikiwemo ukosefu wa Ajira 

 Ameeleza Wizara imeweka Mpango Mikakati Kwa kuunda Timu Maalum ya  watu 14 ambayo itafanya utafiti wa kujua namna Bora ya utafutaji pamoja na uzalisha wa ajira katika sekta binafsi na makampuni .

 Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Uwezeshaji Makame Sufiani amesema Baraza la Vijana lina jukumu kubwa la kuisaidia Serikali hivyo Iko haja ya kuwepo na usahihi wa takwimu kwa Vijana ili kuweza kusaidia Mpango wa  Maendeleo na njia bora ya kuwafikia Vijana hao .

Amesema Baraza la Vijana lina wajibu ya kuisaidia Serikali katika kuimarisha Mabaraza ya Vijana katika ngazi mbali mbali ikiwemo Shehia Wilaya hadi Taifa ili kufikia malengo ya Serikali .

Nae Katibu Mtendaji WA Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan amesema lengo la kuanzisha Mabaraza ya Vijana Zanzibar ni kuhakikisha Vijana wanasaidiwa na kuunganisha kupitia fursa mbali mbali za kiuchumi Kijamii na kiuongozi .

Amesema  Baraza hilo lina jukumu la kuwajenga Vijana wake utaifa na uzalendo ili kuwa raia wema katika kuipenda nchi yao. 

Aidha amesema Muundo wa Baraza la Vijana  Zanzibar umegawika katika sehemu tatu katika ngazi ya Shehia ,Wilaya na Taifa kwa mwanachama yoyote mwenye umri wa miaka 15 hadi 35 kutokana na Sera na Sheria zilizopo pamoja na mikataba ya Afrika ya Vijana.

Amefahamisha kwamba kuna Mabaraza ya Vijana 388 Kwa Unguja na Pemba na Wilaya 11 na ngazi za Taifa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana na Makamu wake na Katibu Mtendaji huteuliwa na Mhe Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk Hussein Ali Mwinyi .

Amesema kutokana na Muundo huo ni sehemu inayowafanya Vijana ushiriki na ushirikishwaji na ni fursa ya kuelezea  changamoto zao na Serikali  kizitafutia ufumbuzi .

Ameeleza kuwa kuwepo kwa Mabaraza hayo ni jambo.la.kujivunia kwa kukusanyika Vijana kujadili Maendeleo yao bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa Kijamii na kiutamaduni ni Moja ya  mafanikio makubwa ya nchi.

Pia amefahamisha mafanikio mengine ya Mabaraza hayo ni kupatiwa sehemu ya kusemea changamoto zao  sambamba na kuwajenga Vijana kiuongozi.




Imetolewa na Kitengo cha Habari 
WVAU

 

Post a Comment