Baraza la Vijana linapatiwa Jengo lenye hadhi Bora ili kutekeleza majukumu yao
Baraza la Vijana linapatiwa Jengo lenye hadhi Bora ili kutekeleza majukumu yao
Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Mhe. Shaaban Ali Othman amesema atahakikisha Baraza la Vijana linapatiwa Jengo lenye hadhi Bora ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa. Ameyasema hayo wakati Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Uwezeshaji walipotembelea Baraza la Vijana Mwanakwerekwe mara baada ya kikao cha kujadili mafanikio na changamoto za Wizara hiyo klichafanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi , Chukwani. Amesema lengo la kuanzisha Wizara ya Vijana ni kuhakikisha Ustawi bora wa Maendeleo ya Vijana unaimarika kwa kuwaletea mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kuwaodoshea changamoto za awali ikiwemo ukosefu wa Ajira Ameeleza Wizara imeweka Mpango Mikakati Kwa kuunda Timu Maalum ya watu 14 ambayo itafanya utafiti wa kujua namna Bora ya utafutaji pamoja na uzalisha wa ajira katika sekta binafsi na makampuni . Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Uwezeshaji Makame Sufiani amesema Baraza la Vijana lina jukumu kubwa la kuisaidia Serikali hivyo Iko haja ya kuwepo na usahihi wa…