YOUTH GROWTH FOUNDATION YAWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA MBALIMBALI
YOUTH GROWTH FOUNDATION YAWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA MBALIMBALI
Na Mwandishi wetu, Geita VIJANA nchini wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali nchini ikiwemo madini, kilimo, ufugaji, teknolojia, uvuvi na ujasiriamali kwani vijana ni ajira. Mkurugenzi mtendaji wa Youth Growth Foundation, Abdul Mzakiru ameeleza hayo kwenye maonyesho ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika manispaa ya Geita. Mzakiru amesema kwenye maonyesho hayo ya Geita wanahamasisha vijana kupitia kauli mbiu yao ya 'Kamata fursa kijanja, madini ni mchongo.' Amesema fursa zipo na zinawasubiri vijana wanaojituma na wanawakaribisha vijana wote kujiunga na Youth Growth Foundation ili waunganishwe na fursa mbalimbali. "Wakijiunga na Youth Growth Foundation tutawawezesha wapate fursa za ajira, mafunzo, biashara, masoko na wadau watakaowasaidia kufikia malengo yao fursa ni kijana, kijana ni ajira," amesema Mzakiru. Ameeleza kuwa taasisi hiyo hutoa fursa za elimu, mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali ili kuwajengea vijana maarifa na ujuzi unaoendana na mahitaji ya…