TBS YAANDAA KLINIKI YA VIWANGO KARIAKOO NA MWENGE
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeandaa kliniki ya viwango katika maeneo ya Soko Kuu la Biashara Kariakoo na Mwenge jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kusogeza huduma za kitaalamu karibu na wafanyabiashara wa bidhaa za chakula na vipodozi ili kuwawezesha kuendesha biashara zinazokidhi viwango. Kliniki hiyo itafanyika kuanzia Septemba 7 hadi 11, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa TBS wa kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi na wafanyabiashara, hususan wanaojihusisha na bidhaa za chakula na vipodozi. Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Usajili wa Bidhaa na Majengo wa TBS, Habakuki Kalebo, amesema wataalamu wa shirika hilo watakuwepo katika maeneo hayo kutoa huduma za ushauri na utaalamu kwa wadau wa sekta hizo. Amesema kliniki hiyo itawapa wafanyabiashara fursa ya kupata elimu kuhusu huduma za usajili wa bidhaa za chakula na vipodozi, pamoja na usajili wa maeneo yanayohusika na uzalishaji, uhifadhi na biashara ya bidhaa hizo. “Lengo kubwa la kliniki hii ni kuhaki…