TANZANIA BIKERS FEDERATION KUANDAA TAMASHA KUBWA LA BIKERS FESTIVAL ARUSHA 2026

TANZANIA BIKERS FEDERATION KUANDAA TAMASHA KUBWA LA BIKERS FESTIVAL ARUSHA 2026
Happy Lazaro,Arusha . Arusha. Tanzania Bikers Federation (TBF) imewataka waendesha pikipiki kubwa na wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki tamasha kubwa la waendesha pikipiki kubwa litakalofanyika jijini Arusha katika eneo la Masai Camp, Oktoba 16 hadi 18 mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arushs Katibu Mkuu wa Tanzania Bikers Federation, Emmanuel Bugabu, amesema tamasha hilo linalenga kuwakutanisha waendesha pikipiki kubwa kutoka maeneo mbalimbali nchini na kuimarisha umoja wao, huku likitumia pia pikipiki kama chombo cha kuelimisha jamii kuhusu usalama barabarani.  Bugabu amesema TBF ni mwavuli unaosimamia maslahi ya waendesha pikipiki kubwa, hususan wenye pikipiki zenye ujazo wa injini kuanzia CC 250 na kuendelea, na kuwa tamasha hilo litakuwa moja ya matukio makubwa ya kuunganisha utamaduni wa waendesha pikipiki bila kulenga mashindano.  Amesema kila mkoa nchini una vilabu vya waendesha pikipiki, ikiwemo Northern Riders na Rock City kutoka Mwanza, Northern Bikers k…