MIVINJENI YAPANUA FURSA ZA ELIMU KWA KUANZISHA LUGHA KICHINA NA KIARABU
MIVINJENI YAPANUA FURSA ZA ELIMU KWA KUANZISHA LUGHA KICHINA NA KIARABU
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHULE ya Mivinjeni Pre and Primary School inatarajia kuanzisha masomo ya lugha ya Kichina na Kiarabu kuanzia mwaka ujao, ikiwa ni hatua inayolenga kupanua wigo wa ujuzi wa lugha kwa wanafunzi na kuwaandaa kukabiliana na mahitaji ya soko la ajira. Akizungumza katika mahafali ya 26 ya shule hiyo, Mkuu wa Shule ya Mivinjeni Pre and Primary School, Sabas Rweichumu, alisema kuanzishwa kwa masomo hayo ni sehemu ya jitihada za kuwapa wanafunzi maarifa na ujuzi utakaowasaidia katika safari yao ya elimu na maisha kwa ujumla. Alisema lugha ya Kichina imepewa kipaumbele kutokana na kuwepo kwa fursa mbalimbali zinazohitaji ujuzi wa lugha hiyo, huku Kiarabu kikitarajiwa kuongeza uwezo wa wanafunzi kujifunza na kutumia lugha zaidi ya moja. Katika mahafali hayo, jumla ya wanafunzi 55 walihitimu elimu ya msingi, huku Rweichumu akieleza kuwa hayo ni mahafali ya kwanza kufanyika tangu shule hiyo ianze kutumia mtaala wa Kiingereza. Akizungumza katika hafla hiyo, mgeni rasmi n…