JAB YASISITIZA USALAMA WA WAANDISHI WAKATI WA MAJANGA
JAB YASISITIZA USALAMA WA WAANDISHI WAKATI WA MAJANGA
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kujiandaa kuripoti majanga yanayoweza kujitokeza katika msimu wa mvua za Vuli, huku wakitanguliza usalama wao, kutoa taarifa sahihi na kuwaelekeza wananchi hatua za kujikinga. Wito huo umetolewa wakati Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ikitabiri kuwa msimu wa mvua za Vuli wa Oktoba hadi Desemba 2026 utaathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Niño. Kwa mujibu wa TMA, mvua za juu ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, ukanda wa Ziwa Viktoria na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma. Akizungumza jijini Dar es Salaam Septemba 21, 2026, Mjumbe wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Bw. Mgaya Kingoba, amesema wananchi hutegemea taarifa za Waandishi wa Habari kufanya maamuzi ya kujilinda wakati wa majanga hivyo, utekelezaji wa jukumu hilo haupaswi kuhatarisha maisha ya Mwandishi. “Wakati wa majanga, Mwandishi wa Habari anatakiwa kutimiza ma…