YAS YAMWEZESHA MTANGAZAJI KURIPOTI AKIWA KATIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

YAS YAMWEZESHA MTANGAZAJI KURIPOTI AKIWA KATIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO
Miaka tisa baada ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mara ya kwanza, mtangazaji wa redio Willy Nkya amepanda tena mlima huo, safari hii akiwa na jukumu la kuripoti matukio kila siku akiwa katika kilele cha mlima huo. Nkya, ambaye alipanda mlima Kilimanjaro kwa mara ya kwanza mwaka 2017 muda mfupi baada ya kumaliza chuo, anasema safari yake ya mwaka huu imekuwa ya tofauti kwa namna kadhaa. Amepanda mlima akiwa na uzoefu zaidi akiwa na maandalizi ya kutosha ya mwili na uelewa mzuri wa namna ya kukabiliana na uchovu, baridi na mabadiliko ya hali ya hewa kadri anavyopanda. Tofauti nyingine kubwa ilikuwa mawasiliano; safari hii ameweza kuwasiliana na kutekeleza majukumu yake ya kikazi katika maeneo mengi ya mlima. Akiwa katika safari hiyo, alitakiwa kurekodi na kutuma video, sauti, picha na taarifa mbalimbali kwa ajili ya matangazo ya redio na mitandao ya kijamii. Anasema mtandao wa Viwango wa Yas ulimwezesha kuendelea kutekeleza majukumu yake katika maeneo mengi aliyopita kuelekea kileleni, huk…