WAZIRI MKUU APONGEZA NMB KWA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIFEDHA VIJIJINI

WAZIRI MKUU APONGEZA NMB KWA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIFEDHA VIJIJINI
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Bi. Vicky Bishubo, alipotembelea banda la benki hiyo katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nanenane yanayoendelea kwenye Viwanja vya John S. Malecela, Nzuguni mkoani Dodoma jana. NMB ni mdhamini wa maonesho hayo. …………..  Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi kupitia matumizi ya teknolojia na mkakati wa Rural Banking, akisema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara na kupunguza gharama za miamala ya kifedha. Akimkaribisha Waziri Mkuu katika banda la NMB kwenye Maonesho ya Nanenane, Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa benki hiyo, Bi. Vicky Bishubo, alisema NMB imeendelea kuwekeza katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji, ikiwa tayari imetoa mikopo yenye thamani ya Sh. trilioni 2.3 kwa sekta hizo. Alisema benki hiyo pia imewawezesha vijana kupata mikopo ya hadi Sh. milio…