WATU 20 WAHOJIWA KUHUSU UCHIMBAJI HARAMU WA MADINI SAME..

WATU 20 WAHOJIWA KUHUSU UCHIMBAJI HARAMU WA MADINI SAME..
SAME. ZAIDI ya watu 20 wanahojiwa na Jeshi la Polisi wilayani Same mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kudaiwa kuendesha shughuli za uchimbaji haramu wa madini katika vyanzo vya maji ndani ya mita 60 kinyume cha sheria na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira. Akizungumza kuhusu hatua zinazochukuliwa jana ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, alisema Kamati ya Usalama ya wilaya ilipata taarifa za siri kuhusu uchimbaji huo katika maeneo mbalimbali na kufika kujiridhisha, ambapo ilibaini kuwepo kwa shughuli hizo. Alisema baada ya kubaini hali hiyo, Kamati iliunda timu ya kwanza ya wataalamu kutoka RUWASA, Bodi ya Maji Bonde la Pangani, Maafisa Mazingira na Maafisa Madini, iliyofanya uchunguzi katika maeneo yote na kubaini uchimbaji haramu katika kata saba pamoja na uharibifu mkubwa wa mazingira. Kasilda alisema kuwa, iliundwa timu ya pili kutoka ndani ya Kamati ya Usalama kwa ajili ya kuwabaini wahusika waliotajwa katika taarifa za siri zilizotolewa na wananchi na baadhi y…