WANAWAKE KATA YA PANGANI WAMPA KONGOLE MWENYEKITI WA UWT KIBAHA MJI KUWANOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

WANAWAKE KATA YA PANGANI WAMPA KONGOLE MWENYEKITI WA UWT KIBAHA MJI KUWANOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI
Na Victor Masangu, Kibaha Baadhi ya wanawake wa (UWT) Kata ya Pangani iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha  wamempongeza kwa dhati Mwenyekiti  wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja  kwa kuamua kutekeleza  aahadi yake kwa vitendo kwa  kufanya ziara maalumu kwa lengo la  kwenda kutoa  mafunzo maalumu  kwa ujasiriamali   ya kuweza  kutengeneza bidhaa za aina mbali mbali ili  kuweweza  kujikwamua kiuchumi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya Mwenyekiti huyo wa UWT Wilaya ya Kibaha Mwenyekiti wa UWT Kata ya Pangani  Johari Komba amebainisha kwamba wamefarijika sana kupata fursa hiyo ya  kupata ujuzi mbali mbali na kufundishwa  jinsi ya kutengeneza bidhaa  tofauti ikiwemo jinsi ya kutengeneza sabuni pamoja na ubunifu wa  batiki. “Kwa kweli sisi kama wanawake wa UWT  kata ya Pangani tunapenda  kumshukuru kwa dhati Mwenyekiti wetu wa Wilaya mama yeetu Elina Mgonja kwa kuweza kuamua kutekeleza ahadi yake kwa vitendo ya kuja kututembelea katika Kata yatu na  haya m…