Wakulima Watahadharishwa Dhidi ya Matumizi ya Mbegu Zisizothibitishwa
Wakulima Watahadharishwa Dhidi ya Matumizi ya Mbegu Zisizothibitishwa
Wakulima wa mahindi nchini wametahadharishwa dhidi ya kutumia mbegu zisizothibitishwa ubora, wakihimizwa kuhakikisha mbegu wanazonunua zimehakikiwa kabla ya kuzipanda ili kuepuka hasara na kupunguza hatari ya kupata mavuno duni. Tahadhari hiyo imetolewa na Bayer Tanzania kupitia kampeni yake ya kitaifa ya uhamasishaji kwa wakulima inayolenga kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kutumia na kuhakiki mbegu halisi kabla ya msimu wa kilimo. Kampeni hiyo inayojulikana kama “DEKALB Mafanikio Shambani” imeendelea Mkoani Morogoro baada ya kuzinduliwa mapema mwezi huu, ikiwa na lengo la kuwafikia wakulima katika maeneo mbalimbali nchini na kuwapatia elimu kuhusu mbegu bora na suluhisho za kisasa za kilimo. Mkurugenzi wa Bayer Tanzania, Sango Mwinyi, alisema matumizi ya mbegu zisizothibitishwa yanaweza kuwaweka wakulima katika hatari ya kupoteza uwekezaji wao, hasa katika kipindi ambacho kilimo kinakabiliwa na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa isiyotabirika. “Wakulima w…