Wajawazito Kunufaika na Teknolojia Nafuu ya UDOM

Wajawazito Kunufaika na Teknolojia Nafuu ya UDOM
Na Mwandishi Wetu  CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM), kupitia Mradi wa SAFARI unaotekelezwa kwa ushirikiano na Liverpool School of Tropical Medicine, kimebuni teknolojia ya matumizi ya akili Unde (Artificial Intelligence) inayolenga kusogeza huduma za uchunguzi wa ujauzito (Ultrasound) karibu na wajawazito wanaoishi katika maeneo yenye upungufu wa wataalamu wa afya. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, mtafiti wa mradi huo, Hamim Rushoke, amesema mfumo huo unatumia kifaa chenye Kumputa na probe maalumu inayowekwa tumboni kwa mjamzito, ambapo akili unde huchambua taarifa na kutoa majibu ndani ya dakika moja bila kuhitaji mtaalamu wa Ultrasound. Amesema kifaa hicho kina uwezo wa kubaini umri wa ujauzito, hali ya uhai wa mtoto, mapigo ya moyo, idadi ya watoto waliopo tumboni pamoja na mkao wa mtoto ikiwa ametanguliza kichwa au miguu, kisha kutoa ripoti ambayo inaweza kusomwa na mhudumu yeyote wa afya. "Teknolojia hii imebuniwa kuondoa chang…