VIONGOZI WAPYA WA TAPSEA WAAPISHWA, WATAKIWA KUSIMAMIA KATIBA YA CHAMA

VIONGOZI WAPYA WA TAPSEA WAAPISHWA, WATAKIWA KUSIMAMIA KATIBA YA CHAMA
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Viongozi wapya wa Chama cha Waandishi Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) wameapishwa rasmi jijini Dar es Salaam, huku wakitakiwa kusimamia Katiba ya chama na kulinda maslahi ya wanachama katika utekelezaji wa majukumu yao. Akizungumza wakati wa kuwaapisha viongozi hao, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franco Kiswaga, aliwataka kuzingatia Katiba ya TAPSEA na kuitumia kama mwongozo katika uongozi wao ili kuhakikisha wanachama wanaongozwa kwa haki na ufanisi. Kiswaga amesema TAPSEA ni chama kikubwa chenye wajibu wa kuwatumikia wanachama wake, hivyo viongozi wanapaswa kuwa imara katika kusimamia maslahi yao na kuhakikisha chama kinaendelea kusonga mbele. “Niwaombe viongozi mnapotoka hapa mkasimamie vyema Katiba yenu ili kuweza kuondoa migogoro itakayojitokeza,” alisema Kiswaga. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa TAPSEA, Leah Mwamba, aliwashukuru wanachama kwa kumpa dhamana ya kuwaongoza na kuahidi kushirikiana nao katika kuh…