VETA YAJIWEKEA MKAKATI WA UJUZI KWA VIJANA KATIKA KUWAFUNGULIA FURSA ZA AJIRA
VETA YAJIWEKEA MKAKATI WA UJUZI KWA VIJANA KATIKA KUWAFUNGULIA FURSA ZA AJIRA
Na Mwandishi Wetu, Tanga MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), CPA Anthony Kasore, amesema mamlaka hiyo imeweka mkakati wa kutoa mafunzo ya ufundi na ujuzi kwa vijana ili kuwafungulia fursa za ajira na kujiajiri katika sekta mbalimbali. CPA Kasore ameyasema hayo alipotembelea Banda la VETA katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga. Amesema VETA ina vyuo katika mikoa mbalimbali nchini, hivyo vijana wanapaswa kutumia fursa hiyo kujiunga na vyuo hivyo na kupata ujuzi unaowawezesha kukabiliana na mahitaji ya soko la ajira. “VETA imejenga vyuo katika kila mkoa na wilaya zake kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi wa maeneo husika, ili kuhakikisha changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi kupitia elimu na mafunzo ya ufundi stadi,” amesema CPA Kasore. Aidha, amesema gharama za mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma kozi ndefu ni Sh 60,000 kwa mwaka kwa wanafunzi wa kutwa, huku wanafunzi wa bweni wakili…