UJENZI WA BARABARA YA LUMECHA-KITANDA-LONDO-MALINYI KUANZA MWAKA HUU
Na Muhidin Amri, Namtumbo SERIKALI imesema,ujenzi wa Barabara ya Lumecha-Kitanda-Londo-Malinyi inayounganisha Mkoa wa Ruvuma na Morogoro kwa kiwango cha lami utaanza mwaka huu wa fedha 2026/2027. Kauli hiyo ya SERIKALI imetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria DKT Juma Homera,amesema hayo Jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mputa,Naikesi na Kitanda wilaya ya Namtumbo wakati wa ziara yake kusikiliza kero na kukagua shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi wilayani Namtumbo. Alisema,serikali tayari imempata mkandarasi kampuni ya China Civil Engneering Co Ltd itakayojenga barabara hiyo ili kurahisisha usafiri,biashara na kufungua fursa mpya za kiuchumi,kijamii na maendeleo kwa mikoa yote miwili na Taifa kwa ujumla. “,Awali mkandarasi alipatikana lakini hakuwa na mtaji,hivyo alishindwa kuanza ujenzi wa barabara hii,lakini sasa Serikali imeamua kujenga kwa fedha zake zenyewe badala ya kusubiri fedha za wafadhili,dhamira ya Serikali ni …