TUME YA MADINI YATOA SIKU 30 KWA MIRADI YA UCHIMBAJI MDOGO YENYE MIKATABA YA MSAADA WA KIUFUNDI KUZINGATIA MATAKWA YA SHERIA YA MADINI

TUME YA MADINI YATOA SIKU 30 KWA MIRADI YA UCHIMBAJI MDOGO YENYE MIKATABA YA MSAADA WA KIUFUNDI KUZINGATIA MATAKWA YA SHERIA YA MADINI
DODOMA, Agosti 26, 2026  Tume ya Madini imetoa muda wa siku 30 kwa wamiliki na wawezeshaji wa miradi ya uchimbaji mdogo yenye Mikataba ya Msaada wa Kiufundi kurekebisha mapungufu yaliyobainika wakati wa ukaguzi, ikionya kuwa itachukua hatua za kisheria, ikiwemo kufuta ridhaa za Msaada wa Kiufundi, kwa watakaoshindwa kutekeleza matakwa hayo. Hatua hiyo inahusu miradi 128 iliyofanyiwa ukaguzi na Tume ya Madini, ambapo miradi 42 ilibainika kutofanya kazi na mingine 86, licha ya kuwa inaendelea na shughuli za uchimbaji, ilibainika kuwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli zake na uzingatiaji wa masharti ya Mikataba ya Msaada wa Kiufundi. Akizungumza jijini Dodoma leo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, amesema Tume imetoa Hati za Makosa zenye muda wa siku 30 kwa wamiliki wa miradi 42 iliyobainika kutofanya kazi, ili watoe mrejesho wa hatua walizochukua kurejesha utekelezaji wa shughuli zao kwa mujibu wa sheria na masharti ya ridhaa za Msaada wa Ki…