TIBA ASILI SALAMA: DKT. NYEMA ATOA WITO WA UTAFITI NA MATUMIZI YENYE USALAMA KWA WANANCHI

TIBA ASILI SALAMA: DKT. NYEMA ATOA WITO WA UTAFITI NA MATUMIZI YENYE USALAMA KWA WANANCHI
Na Atley Kuni, WAF-MBEYA Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Elizabeth Nyema, amewataka wananchi kutumia tiba asili kwa uangalifu na kuhakikisha wanapata huduma kutoka kwa wataalamu wanaotambulika, akisisitiza usalama wa mgonjwa, ubora wa dawa na ushahidi wa kisayansi vinapaswa kuwa msingi wa matumizi na maendeleo ya tiba hiyo. Dkt. Nyema ametoa kauli hiyo Agosti 27, 2026 wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika yanayofanyika nchini kuanzia Agosti 25 hadi 31, 2026, huku kilele cha maadhimisho hayo kikitarajiwa kufanyika Agosti 31 katika Viwanja vya Uhindini, jijini Mbeya. Amesema kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu, “Juhudi katika Utafiti za Tiba Asili katika kuelekea Huduma za Afya kwa Wote,” inalenga kuwakumbusha wananchi na wadau kuwa maendeleo ya tiba asili yanahitaji utafiti, uthibitishaji wa kisayansi na matumizi salama. "Tiba asili ni sehemu ya rasilimali za afya, maarifa ya jamii na urithi wa Watanzania, hivyo ni muhimu kuendelezwa kwa namna inayomlinda mwanan…