TIB YAUNGA MKONO AJENDA YA NISHATI SAFI KUELEKEA DIRA 2050
TIB YAUNGA MKONO AJENDA YA NISHATI SAFI KUELEKEA DIRA 2050
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimkabidhi Tuzo pamoja na Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Deogratius Kwiyukwa, kama Ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kushiriki kukuza na kuchochea shughuli za uchuki jumuishi na shukrani kwa ushiriki na kuwa tayari kuchochea maono ya Taifa ya kumkomboa mwananchi kwa kumtengenezea mazingira bora ya uwajibikaji kwa Taifa lake, katika Kilele cha Tamasha la Kizimkazi 2026, lililohitimishwa mwishoni wa Juma lililopita. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha, Kizimkazi, Zanzibar) Na Benny Mwaipaja, Kizimkazi-Zanzibar SAFARI ya mageuzi ya kiuchumi kuelekea Dira ya Taifa 2050 imeanza kushika kasi, huku mijadala kuhusu vichocheo vya uchumi ikiendelea kupewa uzito mkubwa nchini. Miongoni mwa matukio yaliyoibua mjadala huo ni Tamasha la Kizimkazi 2026, lililofanyika kusini mwa Unguja na kukutanisha viongozi wakuu wa serikali, taasisi na wadau mbalimbali wa mae…