TIA YAWAWEZESHA WAHITIMU KUGEUZA UBUNIFU KUWA FURSA ZA AJIRA

TIA YAWAWEZESHA WAHITIMU KUGEUZA UBUNIFU KUWA FURSA ZA AJIRA
*Nicolaus Mboya ndio Afisa Mtendaji Mkuu wa Sparks 360 Hub Na Mwandishi Wetu, Tanga MHITIMU wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Nicolaus Mboya Mwakampya, amesema mpango wa taasisi hiyo wa kukuza na kuendeleza vipaji na ubunifu umemwezesha kujiajiri na kutoa ajira kwa vijana wengine. Mboya ni miongoni mwa wahitimu wa TIA walionufaika na mpango huo, ambapo ameibua ubunifu wa kiteknolojia unaolenga kuwafundisha watoto matumizi ya teknolojia mbalimbali tangu wakiwa katika ngazi za awali za elimu. Akizungumza katika Maonesho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga, Mboya alisema teknolojia hiyo inalenga kuwajengea watoto uelewa wa teknolojia mapema na hivyo kuongeza idadi ya wataalamu wa teknolojia nchini. Alisema ubunifu wake unahusisha maeneo mbalimbali ikiwemo Robotics, 3D Printing, Electronic Coding, Akili Unde (AI) pamoja na sanaa ya uchoraji. Mboya alisema baada ya kuhitimu TIA, aliendeleza wazo alilolianzisha…