TASAF YAWEKA MKAKATI WA KAYA MILIONI 1.5 KUJITEGEMEA KIUCHUMI NDANI YA MIAKA MITATU

TASAF YAWEKA MKAKATI WA KAYA MILIONI 1.5 KUJITEGEMEA KIUCHUMI NDANI YA MIAKA MITATU
Na Janeth Raphael – MichuziTv MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umeweka mkakati wa kuhakikisha kaya zitakazonufaika na Mpango wa Tatu wa TASAF zinatumia fursa zitakazotolewa kujijengea uwezo wa kiuchumi na hatimaye kuondokana na utegemezi ndani ya kipindi cha miaka mitatu kabla ya kuhitimu kwenye mpango huo. Mpango huo unatekelezwa kwa kipindi cha miaka minne, kuanzia mwaka 2026 hadi 2030, ukiwa na lengo la kubadilisha maisha ya kaya maskini kwa kuzipatia fursa za kuongeza kipato, kuimarisha uwezo wa kujitegemea na kujenga msingi wa maendeleo endelevu, badala ya kuendelea kutegemea msaada kwa muda usio na ukomo. Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Shadrack Mziray, amesema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Zanzibar, iliyotembelea Makao Makuu ya TASAF jijini Dodoma. Mziray amesema mkakati huo unalenga kuhakikisha kaya zinazonufaika na mpango zinatumia ipasavyo fursa zinazotolewa katika kipindi cha miaka mitatu, kabla ya kuhit…