TANZANIA YAUNGA MKONO MABADILIKO YA MFUMO WA AFYA DUNIANI
TANZANIA YAUNGA MKONO MABADILIKO YA MFUMO WA AFYA DUNIANI Na Hassan Kimweri, WAF – Addis Ababa Tanzania imeunga mkono juhudi za kuimarisha Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia maboresho ya Muundo wa Mfumo wa Afya Duniani (Global Health Architecture), huku ikisisitiza umuhimu wa WHO kuendelea kutekeleza jukumu lake la msingi kama mamlaka ya kiufundi ya afya duniani. Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Florence Samizi, amesema hayo leo Agosti 25, 2026 kwenye Mkutano wa 76 wa Kamati ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani (WHO-AFRO), unaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia. “Tanzania inapongeza uongozi wa WHO katika kuratibu ushiriki wa Kanda ya Afrika kwenye utekelezaji wa marekebisho ya Kanuni za Kimataifa za Afya (International Health Regulations – IHR 2024) pamoja na kukamilishwa kwa viambatisho vyake katika Mkataba wa WHO,” amesema Dkt. Samizi Aidha, Dkt. Samizi amesema Tanzania inatambua mchango wa WHO katika kutoa msaada wa kiufundi ili kuimarisha mifumo ya afya, kuboresha ufuatiliaji wa magonjwa, kukabiliana na milipuko, kuendeleza hud…