Posts

TANZANIA YASISITIZA USHIRIKIANO WA UMOJA WA AFRIKA ILI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO

TANZANIA YASISITIZA USHIRIKIANO WA UMOJA WA AFRIKA ILI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO
Na Hassan Kimweri, WAF - Addis Ababa Tanzania imeendelea kusisitiza  ushirikiano wa Umoja wa Afrika (AU) katika kuimarisha juhudi za kupunguza vifo vya mama na mtoto barani Afrika, hususan kupitia utekelezaji wa mikakati na hatua madhubuti zinazolenga kuboresha afya na ustawi wa makundi hayo. Hayo yameongelewa  leo Agosti 25, 2026 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe alipofanya kikao na Kamishna wa Afya, Masuala ya Kibinadamu na Maendeleo ya Jamii wa Tume ya Umoja wa Afrika Mhe. Balozi Amma Twum-Amoah, pembezoni mwa Mkutano wa 76 wa Kamati ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani (WHO-AFRO), unaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Dkt. Magembe amemshukuru Mhe. Balozi Amma Twum-Amoah na Tume ya Umoja wa Afrika kwa ushirikiano  unaoendelea kutolewa kwa Tanzania katika sekta ya afya, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano huo ili kukabiliana na changamoto za afya na kuharakisha hatua za kupunguza vifo vya mama na mtoto barani Afrika. Aidha, Dkt. Ma…