TANZANIA YASHIKA NAFASI YA TATU AFRIKA KWA UBORA WA SEKTA YA MBEGU

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA TATU AFRIKA KWA UBORA WA SEKTA YA MBEGU
Na Scolastica Sambi – MAELEZO Tanzania imeendelea kuthibitisha mafanikio yake katika tasnia ya mbegu baada ya kushika nafasi ya tatu kati ya nchi 55 za Afrika kwa ubora wa sekta ya mbegu, mafanikio yanayotokana na uwekezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita katika utafiti, uzalishaji na uthibiti wa ubora wa mbegu. Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 07, 2026 jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Nyasebwa Chimagu, amesema kuwa Tanzania imepata alama 7.25 kati ya 10 katika tathmini ya The African Seed Access Index (TASAI 2023), ikitanguliwa na Afrika Kusini na Zambia pekee.  “Tanzania inashika nafasi ya tatu kati ya nchi 55 za Umoja wa Afrika kwa ubora wa sekta ya mbegu. Mafanikio haya yanatokana na uwekezaji wa Serikali katika utafiti, uthibiti wa ubora wa mbegu na kuimarisha mifumo ya uzalishaji wa mbegu bora,” amesema Chimagu. Ameongeza kuwa mafanikio hayo yamechangiwa na kuongezeka kwa bajeti ya tasnia ya mbegu kutoka shilingi bilioni 1…