STANBIC YAWA BENKI YA KWANZA TANZANIA KUZINDUA MALIPO YA MOJA KWA MOJA KWA YUAN

STANBIC YAWA BENKI YA KWANZA TANZANIA KUZINDUA MALIPO YA MOJA KWA MOJA KWA YUAN
Kuanzia wa pili kushoto, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Sauda Msemo; Mkurugenzi Mtendaji wa Stanbic Bank Tanzania, Manzi Rwegasira; na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, wakiwa pamoja na wadau wengine wakati wa uzinduzi rasmi wa mfumo wa CIPS na huduma ya malipo ya moja kwa moja kwa Yuan ya China (RMB), jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo unaifanya Stanbic Bank Tanzania kuwa benki ya kwanza nchini kuwezesha wafanyabiashara wanaofanya biashara na China kutuma na kupokea malipo moja kwa moja kwa Yuan, bila kulazimika kubadilisha fedha kupitia Dola ya Marekani. ……………..  Na Mwandishi Wetu DAR ES SALAAM, Tanzania — Benki ya Stanbic Tanzania imekuwa benki ya kwanza nchini kuzindua huduma ya Malipo ya Moja kwa Moja kwa Yuan ya China, inayowawezesha wafanyabiashara wa Tanzania wanaofanya biashara na China kulipa na kupokea malipo kwa Yuan moja kwa moja bila kulazimika kupitia Dola ya Marekani. Kwa mujibu wa taarifa ya Stanbic Tanzania, huduma hiyo inawahudumia waagiza…