SERIKALI YAWEKA MAZINGIRA WEZESHI, WANAWAKE KUTUMIA TEKNOLOJIA NA FURSA ZA BIASHARA KUKUZA UCHUMI

SERIKALI YAWEKA MAZINGIRA WEZESHI, WANAWAKE KUTUMIA TEKNOLOJIA NA FURSA ZA BIASHARA KUKUZA UCHUMI
Na Jackline Minja – WMJJWM, Arusha Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kupitia programu mbalimbali za uwezeshaji wanawake kiuchumi, ikiwemo kuwawezesha kupata mitaji na mikopo kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi.  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, wakati akifungua Kongamano la Usimamizi wa Biashara na Uchumi lililoandaliwa na Wanawake Laki Moja, jijini Arusha, akisisitiza umuhimu wa wanawake kuwa na ujuzi wa kusimamia biashara zao ili ziweze kukua na kuwa endelevu. Naibu Waziri Mahundi amewataka wanawake wajasiriamali kuwa na nidhamu na uwajibikaji kwa kutumia fursa zinazopatikana, ambapo amefafanua kwamba, uwezeshaji wa kiuchumi haupaswi kuishia katika upatikanaji wa mitaji pekee, bali unapaswa kuambatana na maarifa ya usimamizi wa fedha, utunzaji wa kumbukumbu, mipango ya biashara, masoko na matumizi ya teknolojia. “Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais w…