SERIKALI YAKABIDHI PAMPU 52 ZA UMWAGILIAJI WAKULIMA KATAVI KUONGEZA TIJA NA KULINDA MAZINGIRA
SERIKALI YAKABIDHI PAMPU 52 ZA UMWAGILIAJI WAKULIMA KATAVI KUONGEZA TIJA NA KULINDA MAZINGIRA NIRC Katavi. Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imekabidhi pampu 52 za umwagiliaji zenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 500 kwa vikundi 46 vya wakulima mkoani Katavi, ikiwa ni hatua ya kuongeza tija, kupanua eneo linalolimwa na kuimarisha usalama wa chakula. Hafla hiyo ya ugawaji imefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, ambapo mkoa huo umekuwa miongoni mwa wanufaika wa awamu ya kwanza ya mpango huo wa kuimarisha matumizi ya teknolojia ya umwagiliaji katika kilimo. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu, amewataka wanavikundi waliobainishwa kutoyabadilisha matumizi ya vifaa hivyo kwa kuanza kufyatua matofali badala ya kuzalisha mazao. Buswelu amesisitiza kuwa Serikali inalenga kuona wakulima wanaendesha kilimo kinachozingatia hifadhi na utunzaji wa mazingira badala ya kuchepusha au kuiziba mito. Kwa upande wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mkurugenzi Mkuu Bw. Raymond Mndolwa ameeleza kuwa pampu hizo zimetenge…