SERIKALI KUENDELEA KUTOA VIBALI VYA UCHIMBAJI MAENEO YA HIFADHI YANAYORUHUSIWA KISHERIA: DKT. KIRUSWA

*Asisitiza Sheria ya Uhifadhi hairuhusu utafiti, uchimbaji madini mengine isipokuwa Urani, Gesi Asilia na Mafuta *Aeleza Sheria Ya Madini inamtaka Mmiliki wa Leseni Kupata Ridhaa ya Maandishi toka Mamlaka za Hifadhi ya Misitu  Dodoma Serikali imesema itaendelea kutoa Vibali vya Uchimbaji wa Madini katika maeneo ya Hifadhi yanayoruhusiwa Kisheria kwa wananchi na wawekezaji watakaokidhi masharti husika na kupata vibali kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TSF), Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kadri maombi yanavyowasilishwa. Hayo yamebainishwa Agosti 26, 2026 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Steven Kiruswa wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Josephine Kapoma aliyetaka kujua ni lini Serikali itaruhusu wananchi kupewa vibali vya kuchimba madini kwenye hifadhi.  Dkt. Kiruswa amefafanua kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha Sheria ya Misitu, Sura ya 323, uchimbaji wa madini n…