RIDHIWANI: KARAKANA ZIWE CHEMCHEM ZA UBUNIFU, KAZI ZA VIJANA ZISAJILIWE
RIDHIWANI: KARAKANA ZIWE CHEMCHEM ZA UBUNIFU, KAZI ZA VIJANA ZISAJILIWE
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais–Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Mb), Ridhiwani Kikwete, amezitaka shule za msingi na sekondari kuwa na karakana zitakazokuwa chemchemi za ubunifu kwa vijana, huku akisisitiza kazi zitakazobuniwa zisajiliwe ili wabunifu wanufaike nazo. Ridhiwani amesema usajili huo utawasaidia vijana kumiliki kazi zao na kuzitumia kama fursa za kiuchumi, badala ya watu wengine kuchukua mawazo yao na kujinufaisha huku wabunifu wakibaki bila manufaa. Amesema hayo akimwakilisha Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, katika kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Taasisi ya Baobab, iliyopo Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani. Mkurugenzi wa Baobab, Shani Swai, amesema kwa sasa shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 1,000 na tangu mwaka 2007 hadi 2026, jumla ya wanafunzi wa 4,495 wa kidato cha sita wamehitimu, huku asilimia 98 wakiendelea na elimu ya vyuo vikuu ndani na nje ya nchi na wanafunzi 3,270 wamehitimu kidato cha nne ambapo asili…