PSSSF YATOA ELIMU KWA MAKATIBU WA KAMATI ZA BUNGE
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji PSSSF, Bw. Hajji Moshi, akizungumza wakati wa semina maalum ya kutoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Makatibu wa Kamati za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyofanyika mjini Morogoro tarehe 31 Julai, 2026. *Mmoja atoa ushuhuda wa ‘Tunalipa Jana’ *Bunge: tunawashukuru PSSSF kwa elimu Morogoro, Julai 31, 2026 Watumishi wa idara ya Kamati za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameridhishwa na huduma zinatolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa watumishi wa Umma (PSSSF) na wameshauri PSSSF izidishe ubunifu ili kurahisisha huduma kwa Wanachama wake. Kauli hiyo imetolewa Julai 31, 2026 mjini Morogoro katika semina iliyoendeshwa na PSSSF maalum kwa Watumishi wa Bunge ambayo iliwashirikisha Makatibu wote wa kamati za Bunge. Semina ilikuwa ya kuwajengea uwelewa wa Kinga ya Jamii, hususani PSSSF. “Hongereni sana matumizi ya mtandao hivi sasa mambo mmeyarahisisha sana, kwani kila kitu kinaanzwa na kumalizwa kwenye simu au kifaa kingine chochote cha k…