ORYX GAS ZANZIBAR YAKABIDHI MITUNGI YA GESI 200 KIZIMKAZI

ORYX GAS ZANZIBAR YAKABIDHI MITUNGI YA GESI 200 KIZIMKAZI
ORYX Gas Zanzibar imeeleza hatua mbalimbali inazochukua kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na katika Tamasha la Kizimkazi kampuni hiyo imetoa mitungi ya gesi 200 huku mkakati kwasasa ni kutoa majenerata yanatotumia gesi ya LPG katika hoteli na viwanda visiwani Zanzibar. Imesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika matumizi ya LPG na kwamba katika kipindi cha miaka sita matumizi ya nishati safi ilikuwa asilimia sita mwaka 2020 lakini mwaka 2025 ni zaidi ya asilimia 30 ya watumiaji wa nishati safi ya kupikia ya gesi na muamko huo umechangiwa na sekta binafsi,Serikali na wadau wengine. Akizungumza katika kongamano la nishati safi lililofanyika wakati wa Tamasha la Kizimkazi Zanzibar lililoanza Agosti 12 na kuhitimiswa leo Agosti 14,2026, Meneja Mkuu wa Oryx Gas Zanzibar Shuwekha Khamis amesema kampuni hiyo Oryx wanamchango mkubwa katika matumizi ya nishati safi ya kupikia. “Hii kazi tumeianza muda mrefu na tumekuwa tukizisaidia taasisi katika mabadiliko na hapa Zanzibar oryx tum…