NIT YAZALISHA WATALAAMU WA SGR NA USAFIRI WA MAJINI
NIT YAZALISHA WATALAAMU WA SGR NA USAFIRI WA MAJINI Na Baraka Messa – MAELEZO Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimesema kinaendelea kupanua wigo wa mafunzo kwa kuanza kuzalisha wataalam wa kada mbalimbali katika sekta ya usafirishaji na miundombinu ikiwemo ya SGR na usafiri majini hatua inayolenga kukidhi mahitaji na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika miradi ya kimkakati nchini. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26, Agosti 3, jijini Dodoma Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Dkt. Prosper Mgaya, amesema awali NIT kilijikita zaidi katika kuzalisha madereva wa usafiri wa barabarani, lakini sasa kimebadilika na kuwa taasisi inayotoa wataalam wa nyanja mbalimbali za usafirishaji. Amesema uwekezaji uliofanywa na Serikali katika miundombinu ya kisasa, ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR), umewezesha chuo kuanzisha programu za diploma na shahada ya kwanza zinazolenga kuzalisha wataalam watakaohudumia sekta hiyo muhimu ya uchumi. “Awali NIT ilijikita zaidi kutoa wata…