NDEJEMBI AAPISHWA IKULU! RAIS SAMIA ASEMA 'NAFASI IMEKABIDHIWA KWA KIJANA KAWATUMIKIE WATANZANIA BILA KUJALI TOFAUTI ZAO'
NDEJEMBI AAPISHWA IKULU! RAIS SAMIA ASEMA 'NAFASI IMEKABIDHIWA KWA KIJANA KAWATUMIKIE WATANZANIA BILA KUJALI TOFAUTI ZAO'
Na Janeth Raphael - MichuziTv -Ikulu Chamwino Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema uamuzi wa kumteua Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais ulizingatia sifa, uzoefu na uwezo wake wa kubeba dhamana kubwa ya uongozi wa taifa. Rais Samia amesema nafasi hiyo imekabidhiwa tena kwa kijana, akimtaka Ndejembi kutumia fursa hiyo kujifunza, kukua kiakili na kutekeleza majukumu yake kwa weledi, utii na uaminifu kwa maslahi ya Watanzania. Akizungumza leo, Agosti 29, 2026, katika hafla ya kumuapisha Ndejembi kuwa Makamu wa Rais iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma, Rais Samia amesema uamuzi wa kumrudisha kijana katika nafasi hiyo ulifanyika kwa kauli moja. “Kwa kauli moja tuliamua kuirudisha nafasi ya Makamu wa Rais kwa vijana na tuendelee kulea. Imetoka kwa kijana na tumeirudisha kwa kijana. Tunakuomba kijana (Ndejembi) ukakue sio kwa umri bali ukakue kiakili, tumekupa majukumu makubwa ni imani yangu utaweza,” amesema Rais Samia. Rais Samia amesema Ndejembi alipat…