MIRADI YA ZAIDI YA MILIONI 644 YATEKELEZWA NAMTUMBO HOMERA AMSHUKURU RAIS SAMIA
MIRADI YA ZAIDI YA MILIONI 644 YATEKELEZWA NAMTUMBO HOMERA AMSHUKURU RAIS SAMIA
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Juma Zuberi Homera akizungumza na wananchi wa Namtumbo wakati wa ziara yake ambayo imeanza jana katika kata za Hanga na Mputa Namtumbo ikilenga kukagua miradi yenye thamani ya shilingi milioni 644 na kusikiliza kero za wananchi Moja ya mawe yaliyowekwa na Mbunge wa Jimbo la Namtumbo na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Juma Zuberi Homera Na Regina Ndumbaro Namtumbo Mbunge wa Jimbo la Namtumbo na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Zuberi Homera, amesema wananchi wa Namtumbo wanaendelea kushuhudia maendeleo makubwa kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha za miradi hiyo. Dkt. Homera ameyasema hayo Agosti 12, 2026, wakati wa ziara yake ya kikazi katika kata za Hanga na Mputa, ambapo alikagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 644, huku akisikiliza ke…