MEYA IRINGA: MITAMBO YA KISASA YA MACHINJIO YA NGELEWALA YAWASILI YAANZA KUFUNGWA
MEYA IRINGA: MITAMBO YA KISASA YA MACHINJIO YA NGELEWALA YAWASILI YAANZA KUFUNGWA NA DENIS MLOWE IRINGA MEYA wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada, amesema Serikali imefanikisha hatua kubwa ya kukamilisha ujenzi wa Machinjio ya Kisasa ya Ngelewala baada ya mitambo ya kisasa ya kuchinjia ng’ombe, mbuzi na kondoo kuwasili na kuanza kufungwa. Ngwada amesema mitambo hiyo imenunuliwa kwa fedha zilizotolewa na Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambapo Manispaa ya Iringa ilipokea Sh bilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa mitambo hiyo. Amesema kati ya fedha hizo, Sh milioni 920 zimetumika kuingia mkataba na kampuni ya Jipco kwa ajili ya ununuzi na ufungaji wa mitambo hiyo, huku akiwataka wananchi wa Iringa kutambua kuwa mradi huo ni halisi na unaendelea kutekelezwa. “Mheshimiwa Rais katuletea pesa na tumefanya ununuzi wa vifaa ambavyo leo Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa tumekuja kuvipokea rasmi,” amesema Ngwada. Amesema awali Serikali ilitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika eneo hilo, i…