MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI YAINGIA KUMI BORA TAMASHA LA UTAMADUNI KITAIFA

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI YAINGIA KUMI BORA TAMASHA LA UTAMADUNI KITAIFA
NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO Mashindano ya Ngoma za Asili yameendelea kwa hamasa katika Tamasha la Nne la Utamaduni linalofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro huku mikoa 10 ikifanikiwa kuingia katika hatua ya kumi bora. Mikoa iliyofanikiwa kuingia katika hatua hiyo ni Mbeya, Mwanza, Morogoro, Pwani, Mtwara, Dodoma, Njombe, Arusha, Lindi na Dar es Salaam. Mashindano hayo ni miongoni mwa matukio yanayovutia katika tamasha hilo yakilenga kuonyesha utajiri wa mila, desturi na sanaa za asili zinazopatikana katika jamii mbalimbali nchini Tanzania. Washiriki kutoka mikoa hiyo wameonesha umahiri mkubwa kupitia ngoma zao za asili, wakitumia midundo, nyimbo, mavazi na miondoko ya jadi kuwasilisha historia na utamaduni wa jamii zao. Akizungumza baada ya kufanikiwa kuingia katika hatua ya kumi bora, Mwajuna Omary mshiriki kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, amesema juhudi, maandalizi na ushirikiano wa washiriki wa kikundi chake vimekuwa miongoni mwa sababu zilizowafikisha katika hatua hiyo. Amese…