MALIMA AFUNGUA TAMASHA LA UTAMADUNI KITAIFA, AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA AFCON KUTANGAZA TAMADUNI KAMA VIVUTIO ADIMU
MALIMA AFUNGUA TAMASHA LA UTAMADUNI KITAIFA, AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA AFCON KUTANGAZA TAMADUNI KAMA VIVUTIO ADIMU
Farida Mangube Morogoro Serikali imewataka watanzania kuitumia vizuri fursa ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON 2027 kwa kutangaza tamaduni za makabila mbalimbali kama sehemu ya vivitio adimu vinavyopatikananchini humo sambamba na kufanya vizuri kwenye michezo hiyo. Kauli hiyo Imetolewa na Mkuu wa Mkoa Morogoro,Adam Malima wakati akifungua Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika mjini Morogoro ambapo jumla ya wahiriki 150,000 kutoka mikoa mbalimbali wanaonyesha tamaduni.zao. Amesema katika michuano hiyo licha ya Tanzania kushiriki nchi zingine ni Kenya na Uganda ambazo zinaendelea na maandalizi ya michezo hiyo ambapo kwa Tanzania itafanyika Arusha,Dar es salaam na Zanzibar. Aidha amewataka watanzania kuendelea kuheshimu utamadani kwani bila kuwepo Kwa utamaduni huwezi kuwa na heshima. Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema tamasha Hilo la Kitaifa la Utamaduni lilianzia Mkoani Dar Salaam,likaenda …