KURASINI EXTENSION KUPUNGUZA FOLENI YA MALORI BANDARI YA DAR ES SALAAM
KURASINI EXTENSION KUPUNGUZA FOLENI YA MALORI BANDARI YA DAR ES SALAAM
Na Sheila Ahmadi, Dar es Salaam Serikali imeeleza kuwa eneo la Kurasini Extension linatarajiwa kuanza kutumika kama sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam ifikapo Novemba mwaka huu, hatua inayolenga kupunguza msongamano wa mizigo na malori katika Bandari ya Dar es Salaam. Eneo hilo linatarajiwa kutumika kama Port Extension, ambapo mizigo itakayoshushwa katika Bandari ya Dar es Salaam itaelekezwa Kurasini Extension kwa ajili ya kuhifadhiwa, kukaguliwa na kusambazwa kwa maeneo mbalimbali. Akizungumza Jijini Dar es salam Mara baada ya kutembelea bandari kavu iliyopo Kurasini Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Kurasini Extension linatarajiwa kuwa na uwezo wa kuhudumia hadi makasha 700,000 kwa mwaka, ikilinganishwa na uwezo wa sasa wa Bandari ya Dar es Salaam wa kuhudumia takribani makasha 344,000 kwa mwaka. Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza uwezo wa bandari kuhudumia shehena kwa ufanisi, huku sehemu kubwa ya shughuli za mizigo ikihamishiwa katika eneo hilo na hivyo kupunguza…