KIKWETE ATEMA CHECHE AWAHIMIZA WALIMU WA BAOBAB KUCHAPA KAZI KWA MASLAHI YA TAIFA
KIKWETE ATEMA CHECHE AWAHIMIZA WALIMU WA BAOBAB KUCHAPA KAZI KWA MASLAHI YA TAIFA
Na Victor Masangu,Bagamoyo WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais–Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete, amewataka walimu wa shule za msingi na sekondari kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na weledi lengo ikiwa ni kuweza kuzalisha wanafunzi wenye ujuzi na maarifa ambao watalisaidia Taifa katika nyanja mbali mbali. Ridhiwani ameyabainisha hayo alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Taasisi ya Shajar ambayo inamiliki shule ya Baobab iliyopo Wilaya ya Bagamoyo. Amesema kwamba katika Taifa la Tanzania walimu wa shule za msingi na sekondari wana mchango mkubwa sana hivyo wanapaswa kufanya kazi zao katika misingi imara ambayo itaweza kusaidia kupata wataalamu bora. Pia Ridhiwani amesema ameridhishwa na ubunifu unaofanywa na wanafunzi wa shule hiyo na kusisitiza kuwa kazi zao wanazozifanya kulindwa na kusajiliwa. Amesema kwamba uongozi wa Taasisi hiyo wanapas…