ITA YATUMA MAONYESHO YA WIKI YA ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU KUTOA ELIMU

ITA YATUMA MAONYESHO YA WIKI YA ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU KUTOA ELIMU
Na Mwandishi Wetu, Tanga CHUO cha Kodi (ITA) kimeshiriki Maonesho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara jijini Tanga, kwa kutoa elimu kuhusu majukumu ya Chuo hicho pamoja na fursa za mafunzo zinazotolewa. Wanafunzi na wadau mbalimbali waliotembelea banda la ITA wamepata fursa ya kufahamu kwa kina kuhusu programu za mafunzo zinazotolewa na Chuo hicho, huku wakihamasishwa kujiunga na mafunzo hayo. Maonesho hayo yaliyoanza Agosti 15, 2026, yamekuwa pia jukwaa kwa ITA kuwaelimisha wananchi kuhusu nafasi ya taaluma mbalimbali katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na maeneo mengine ya ajira. Akizungumza na wanafunzi waliotembelea banda hilo, Afisa Mkuu wa Uhusiano wa Umma wa ITA, Oliver Njunwa, amesema mwanafunzi anayelenga kufanya kazi TRA anapaswa kuzingatia masomo yote kwa kuwa Mamlaka hiyo inaajiri wataalamu wenye taaluma mbalimbali. “TRA ina wafanyakazi wenye taaluma mbalimbali, hivyo mwanafunzi anatakiwa kuzingatia masomo yote na kufanya vizuri katik…