‎IOM DUNIANI NA UHAMIAJI TANZANIA WAZINDUA MFUMO WA URATIBU WA KITAIFA (NCM) KUHUSU UHAMIAJI NCHINI TANZANIA

‎IOM DUNIANI NA UHAMIAJI TANZANIA WAZINDUA MFUMO WA URATIBU WA KITAIFA (NCM) KUHUSU UHAMIAJI NCHINI TANZANIA
‎Na Konstebo Nangigi Mohamed, Dodoma. ‎ ‎Mfumo wa Uratibu wa Uhamiaji Kitaifa kati ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) Duniani na Idara ya Uhamiaji Tanzania umezinduliwa leo tarehe 18 Agosti 2026, Katika Hafla iliyofanyika Katika ukumbi wa Mabeyo Hall Jijini Dodoma huku ukiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano, uratibu na ufanisi katika usimamizi wa masuala ya uhamiaji nchini, pamoja na kuimarisha diplomasia na kukuza uchumi. ‎ ‎Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Patrobas Katambi (Mb) ambae alikuwa Mgeni Rasmi amesema Tanzania inathamini mchango na ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kusimamia masuala ya uhamiaji, hususan IOM, ambayo ni miongoni mwa washirika muhimu. ‎ ‎“Tanzania inathamini ushirikiano na wadau mbalimbali, wakiwemo IOM, katika kuhakikisha tunaimarisha mifumo na uwezo wa kusimamia uhamiaji kwa ufanisi. Uhamiaji unajumuisha afya, maendeleo, ajira, mitaji na usalama wa kitaifa. Haya yote yafanyike bila kuathiri usalama, utu na heshima …